


...................
NA MUSSA KHALID,NAIVASHA KENYA
Wawakilishi kutoka Huduma za Kitaifa za Hali ya Hewa
(NMHSs),Mashirika ya Kiraia,sekta binafsi pamoja waaandishi wa habari wamesisitizwa
kwenda kufanya taarifa na usambazaji wa huduma za taarifa za hali ya hewa ili
kuisaidia jamii kuepukana na majanga.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwanasayansi wa utafiti wa
Hali ya Hewa kutoka Kituo cha IGAD cha Utabiri na Matumizi ya Tabianchi Titike
Bahaga wakati akizungumza kwenye warsha maalamu ya siku tano ambayo
imewakutanisha wadau katika Kaunti ya Nakuru,Mji wa Naivasha Nchini Kenya.
Bahaga amesema kuwa malengo ya kuwakutanisha wadau hao
ni kuwaongezea uelewa na utumiaji wa huduma za hali ya hewa kwa
ajili
ya ufuatiliaji wa hatari za kikanda, kutafsiri taarifa za hatari, na kusaidia
mawasiliano na kufanya maamuzi.
"Tunaamini kwamba kama programu na mradi huu tunawekeza katika kutoa
mafunzo kwa wanahabari kutoka vyombo mbambali ngazi ya kitaifa ikiwa ni kwa
eneo muhimu la kueneza habari za hali ya hewa kwa jamii"
Kwa upande wake Mkufunzi wa wanahabari kutokea nchini Kenya Mr Issac Sagala
lengo ni kupanga mikakati ya pamoja ili kuboresha ushirikiano na wadau kutoka
katika sekta mbalimbali kupata taarifa zitakazosaidia kukabiliana na mabadiliko
ya hali ya hewa.
Amewasisitiza wanahabari kudhibiti taarifa na kutoa taarifa ambazo
zimethibitishwa na Mamlaka za Hali ya hewa ili kutoleta sintofahamu kwa jamii
hasa za vijijini.
Katika warsha hiyo imejadiliwa namna na ushiriki na kuwalinda watoto katika
masuala ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi ambapo Meneja kutoka Shirika
la Save the Children Mary Chavula amesema kuwa wamefundisha ni kwa namna gani
wazazi na jamii nzima wanapaswa kuwalinda watoto.
Amesema kuwa zimekuwa zikitumika mbinu mbalimbali za kuwafunza watoto ikiwa
ni pamoja na vyombo vya habari Radio,Tv na katika mitandao ya kijamii ili
waweze kuwa vinara katika masuala ya hali ya hewa.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika warsha hiyo akiwemo Mwanahabari
wa KIGALIINFO kutoka nchini Rwanda Saimon Kamuzinzi pamoja na Mwanahabari
kutoka SIFA FM ya nchini Kenya Linda Akothi wamesema kuwa walichojinza ndio
ushirikiano unaohitajika ili kuhakikisha habari wanazozitoa za kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi yanawafaa zaidi wanaposhirikiana.
Aidha Linda amesema kuwa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi watoto
wameathirika pakubwa hivyo warsha hiyo imeonyesha taswira kamili kuwa kuna
uhitaji mkubwa wa washika dau kuwashirikisha ikiwemo kutengeneza habari
zitakazowasaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Warsha hiyo ya siku tano imeyakutanisha mataifa manne ya Afrika Mashariki
ikiwemo Tanzania,Rwanda,Burundi na Kenya ambao wamekuwa ni wenyeji
imeratibiwa
na Kituo cha IGAD cha Utabiri na Matumizi ya Tabianchi (ICPAC), kwa
ushirikiano na UK Met Office and Norwegian Capacity (NORCAP), kupitia mradi wa
Uimarishaji wa Msimu wa Afrika Mashariki - Afrika Mashariki (PASS-EA) chini ya
Mpango wa WISER Africa unaofadhiliwa na Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya
Madola na Maendeleo ya Uingereza (FCDO) ambapo imelenga kuboresha ubora,
ufikiaji, na matumizi ya taarifa za hali ya hewa.



.jpeg)
.jpeg)







.jpeg)
.jpeg)
Chapisha Maoni