..................
NA MUSSA KHALID
Timu ya Simba SC imeendelea kujitika kileleni mwa
msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga timu ya JKT Tanzanzia kwa
jumla ya goli moja kwa sifuri (1-0).
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ugumu kwa kila
pande kutokubali nyavu zake kutikishwa alilazimu mpaka dkk za nyongeza ambazo
zikaifanya Simba kupata mkwaju wa Penati iliyofungwa na mchezaji wake Jean
Ahoua.
Hata hivyo matokeo hayo yanaifanya timu ya Simba kufikisha alama 37 baada ya kucheza michezo 14 huku timu ya JKT ikisaliwa na alama 19 baada ya kucheza michezo 15.
Chapisha Maoni