Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt.
Natu El-maamry Mwamba, akijadili kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika
kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na
kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha
miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management
of Eastern and Southern Africa (MEFMI), mjadala uliofanyika kando ya Mikutano
ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika
Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani. Katikati ni
mwongoza majadiliano (Moderator) ambaye ni Waziri wa Fedha wa Uganda, Dkt.
Ramathan Ggoobi, na kulia ni Mtoa Mada, Bw. Reginald Max, ambaye ni Mshauri
Mwandamizi wa masuala ya Miundombinu na Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi Kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo (TDB).
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt.
Natu El-maamry Mwamba, akijadili kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika
kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na
kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha
miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management
of Eastern and Southern Africa (MEFMI), mjadala uliofanyika kando ya Mikutano
ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika
Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt.
Natu El-maamry Mwamba (katikati), akiteta jambo na Waziri wa Fedha wa Uganda,
Dkt. Ramathan Ggoobi (kulia), na Mshauri Mwandamizi wa masuala ya Miundombinu
na Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi Kutoka Benki ya Biashara na
Maendeleo (TDB), Bw. Reginald Max, baada ya kushiriki mjadala (Panelists)
kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta rasilimali fedha kwa
ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na
mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 30 tangu
kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management of Eastern and
Southern Africa (MEFMI), mjadala uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya
Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika Hoteli ya
Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Mawaziri wa Fedha, Makatibu Wakuu na
Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi za Afrika, wakiwa katika picha ya pamoja
wakati wakiadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and
Financial Management of Eastern and Southern Africa (MEFMI), maadhimisho
yaliyoambatana na mjadala kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta
rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii
zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, mjadala uliofanyika kando ya Mikutano
ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika
Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt.
Natu El-maamry Mwamba, wakiwa katika picha na Waziri wa Fedha na Maendeleo wa
Lesotho, Dkt. Retselisitsoe Adelaide Matlanyane (Mb), katika hafla ya
kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and
Financial Management of Eastern and Southern Africa (MEFMI), maadhimisho
yaliyoambatana na mjadala kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta
rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii
zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, mjadala uliofanyika kando ya Mikutano
ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika
Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha, Washington D.C, Marekani)
.........................
Na Benny Mwaipaja, Washington D.C, Marekani
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ametoa wito kwa Benki Kuu za Nchi za Afrika, kuweka mipango na mikakati ya kutafuta fedha kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta binafsi kwa ajili ya kukabiliana na athari hasi za mabadiliko ya tabianchi katika nchi hizo.
Dkt. Mwamba ametoa rai hiyo wakati akishiriki mjadala kuhusu wajibu wa Benki Kuu za nchi za Afrika kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Macroeconomic and Financial Management of Eastern and Southern Africa (MEFMI), mjadala uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), katika Hoteli ya Mayflower, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Alisema kuwa mbinu mahususi ikiwemo uanzishwaji wa hati fungani za kijani zenye lengo la kuvutia uwekezaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na kusimamia ipasavyo Taasisi za fedha kuwekeza kwenye kilimo kwa kutoa mikopo, zitasaidia kukuza uchumi wa nchi hizo za Afrika na maendeleo ya watu wake.
Dkt. Mwamba alibainisha katikaTukio hilo lililowakutanisha Mawaziri wa Fedha, Makatibu Wakuu na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi za Afrika, kwamba mabadiliko ya tabianchi yameziathiri nchi nyingi ikiwemo Tanzania na kwamba upatikanaji wa fedha kwa njia shirikishi katika kukabiliana na athari hizo kutaimarisha uchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MEFMI, Dkt. Louis Kasekende, alisema kuwa Taasisi yake imejipanga kuwawezesha wanachama wake kuweka mipango ya pamoja ya kutafuta fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na usimamizi wa uhimilivu wa madeni ya nchi za Afrika.
Mbali na Dkt. Mwamba, washiriki
wengine katika mkutano huo kutoka Tanzania, walikuwa Naibu Katibu Mkuu
anayesimamia Sera za Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.

Chapisha Maoni